Ephesians 5:8-14

8 aKwa maana zamani ninyi mlikuwa giza, lakini sasa ninyi ni nuru katika Bwana. Enendeni kama watoto wa nuru 9 b(kwa kuwa tunda la nuru hupatikana katika wema wote, haki na kweli), 10 cnanyi tafuteni yale yanayompendeza Bwana. 11 dMsishiriki matendo ya giza yasiyofaa, bali yafichueni. 12 eKwa maana ni aibu hata kutaja mambo yale ambayo wasiotii wanayafanya sirini. 13 fLakini kila kitu kilichowekwa nuruni, huonekana, 14 gkwa kuwa nuru ndiyo hufanya kila kitu kionekane. Hii ndiyo sababu imesemekana:

“Amka, wewe uliyelala,
ufufuke kutoka kwa wafu,
naye Kristo atakuangazia.”
Copyright information for SwhNEN